24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ULEGA APIGIA CHAPUO TEHAMA MKURANGA

Na ASHA  BANI-DAR ES SALAAM


NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amesema kuanzishwa kwa mradi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kutasaidia kukuza uchumi wa nchi.

Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, amesema mradi huo ambao ulianzishwa na Kampuni ya Raddy Fibre Solution (LTD) unatarajiwa kutandaza mkongo wa Taifa katika wilaya 185 ikiwemo Mkuranga

Akizungumza na ujumbe wa kampuni hiyo mwishoni mwa wiki wilayani Mkuranga, alisema kukamilika kwa mfumo huo kutaisadia wafanyabiashara wenye viwanda kujua hali ya masoko ya ndani na nje haraka.

“Hivi sasa serikali ipo katika harakati za kukuza uchumi kupitia viwanda na kama mnavyofahamu Mkuranga ni eneo maalumu la kimkakati la viwanda ambalo linatakiwa kuwa na mawasiliano ya uhakika.

“Ufungwaji wa mfumo huu Wilaya ya Mkuranga utaiunganisha wilaya yetu, wamiliki wa viwanda pamoja na wana Mkuranga,” alisema Ulega

Hivi karibuni  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Mhandisi Mshamu Munde akiwa katika mkutano wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ALAT) alisema hatua za awali za mpango huo zitakuwa na manufaa kiuchumi.

Alisema mfumo huo ambao unafahamika kama e-LGA unafanana na mfumo wa Serikali Mtandao (e-Gorvement) hivyo utasaidia kufanya kazi za mawasiliano kwa urahisi zaidi.

“Imefika wakati sasa kwa wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutumia mfumo huo kwa kuwa utakuwa na manufaa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hasa kwa ngazi za halmashauri.

“Pia utakuwa na manufaa zaidi hasa kusaidia kurahisisha mpango wa malipo, kuingiza taarifa za afya za wilaya na hata shughuli za kiuchumi kama vile kilimo na mifugo na mifumo mingineyo

“Utasaidia kuunganisha masoko kwa wafanyabiashara, wakulima wa nyanya Iringa kuweza kufanya biashara na wakulima wa mpunga Mbeya na Korosho Mkuranga kwa kuwasiliana kupitia mkongo wa mawasiliano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles