Ulaji wa kupitiliza husababisha saratani

0
654

AVELINE KITOMARY -DAR ES SALAAM

MTAALAMU wa lishe kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Brenda Maro, amesema watu wenye mazoea ya kula kupita kiasi wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa saratani.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu jana Dar es Salaam, Brenda alisema ulaji wa kupitiliza, hasa wa vyakula yenye mafuta na kemikali, kwa kiasi kikubwa ndio unachangia mtu kupata saratani.

“Mazoea ya kula kupita kiasi yanaweza kupelekea uzito mkubwa baadaye, hasa sehemu kubwa ya vyakula ikiwa ni vya mafuta mengi, vyakula vya kusindikwa na aina mbalimbali za kemikali ni moja ya hatari ya maradhi kama vile saratani.

“Ila pia eneo kubwa ikiwa ni wanga, mtu ‘ana-overwork’  kongosho ambalo kazi yake kubwa ni kuachilia ‘insulin’ inayotumika kupeleka ‘glucose’ kwenye ‘cell’, hivyo kupelekea kulichosha.

“Kongosho huwa ina kazi kubwa ya ‘ku-control blood sugar’, kwahiyo ikiwa haifanyi kazi yake ipasavyo, sukari hubaki nyingi katika damu,” alifafanua Brenda.

Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Hellen Makwani, aliunga mkono kauli hiyo akisema kuwa ulaji kupita kiasi unaweza kusababisha uzito kuongezeka.

Alisema uzito ukiwa mkubwa mara nyingi ni rahisi mtu kupata saratani ya kongosho na saratani ya utumbo.

“Kuna uhusiano wa hivyo vitu, uzito ukipitiliza ni hatari, mtu anaweza akapata saratani ya kongosho au hata ya  utumbo, kwa mfano hao wanaokula sana vyakula vya mafuta wako hatarini zaidi,” alisema Dk. Makwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here