Ukarabati mnara Zinjathroupus waanza

0
1053

Ferdnanda Mbamila -Dar es salaam

HATIMAYE agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kukarabati miundombinu na ujenzi wa mnara wa Zinjathropus boisen katika bonde la Olduvai limeanza kutekelezwa.

Majaliwa alitoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya uzinduzi wa fuvu la binadamu wa kwanza duniani Zinjathropus boisen Julai 22, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam juzi, Meneja Idara ya Urithi wa Utamaduni wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Joshua  Mwankunda, alisema eneo la Olduvai linatarajia  kuwekewa mnara ili kuonyesha maelezo na mwongozo wa wageni mbalimbali, hasa wanafunzi  na watalii, wanaokwenda kutalii na kujifunza.

 “Tumefanya ukaguzi wa eneo hili jinsi barabara itakavyopita kwenda kwenye vivutio vilivyopo bila kuathiri maeneo mengine,” alisema.

Mwankunda alisema katika uboreshaji wa eneo hilo, tayari vijana wawili wamepewa mafunzo ya namna ya kuelekeza wageni.

Alisema lengo la ujenzi wa mnara wa Zinjathropus, ni kushawishi watu kufika eneo hilo na kujionea jinsi binadamu wa kwanza alivyopatikana.

 “Tumebuni mchoro na kutambua eneo maalumu ambalo limeandaliwa kwa ujenzi wa jengo la chakula katika nyumba ya makumbusho aliyokuwa akiishi mgunduzi wa fuvu, Dk. Mery Leaky,” alisema.

Mwankunda alisema maagizo mengine ya Majaliwa, ni pamoja na kutunza rasilimali na watashirikiana na wizara husika.

Alisema lengo ni kuhakikisha rasilimali zinalindwa, zinatuzwa na kunufaisha jamii ya Watanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here