28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Kabendera yapigwa kalenda

Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera (39), anayekabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutakatisha zaidi ya Sh milioni 173, ataendelea kusota rumande hadi Agosti 30 mwaka huu kesi yake itakapotajwa.

Shauri hilo limetajwa leo Jumatatu Agosti 19, saa tatu asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Mmbando kwa sababu Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile anayesikiliza kesi hiyo kuwa na udhuru.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi ilikuwa inatajwa na upelelezi haujakamilika wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30 mwaka huu kwa kutajwa, mshtakiwa ataendelea kuwa rumande.

Katika shauri hilo, Kabendera na wenzake ambao hawapo mahakamani alitoa msaada kwenye genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia fedha, kukwepa kodi ya Sh milioni 173 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutakatisha kiasi hicho cha fedha huku akijua zimetokana na zao la kusaidia genge la uhalifu na kukwepa kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles