23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Uhusiano kati ya baba wanene, binti zao kupata saratani

Tipped the Scale Weight Loss

Na Joseph Hiza,

UTAFITI mpya umeonya kuwa akina baba wenye unene au uzito mkubwa wanawaweka binti zao katika hatari ya kupata saratani ya matiti.

Wanasayansi wanasema binti hao wenye baba wanene lakini mama wembamba huzaliwa na uzito mkubwa, ambao huendelea kuwa nao kipindi chote cha utoto wao.

Pia hali hiyo huchelewesha ukuaji wa tishu katika matiti yao pamoja na kuongeza uwezekano wa kupata saratani ya titi.

Utafiti huo ulikuwa wa kwanza kuangazia athari za mwanamume wanene kwa watoto wanaozaliwa juu ya uwezekano wa kupata saratani katika siku za usoni.

Na utafiti huo unabainisha kuwa kubeba uzito wa ziada hubadili vinasaba (DNA) vya mbegu za kiume za mwanamume, hali ambayo huathiri afya ya binti mtarajiwa.

Unene hubadili taswira za ‘microRNA (miRNA)’, epijenetiki (epigenetic) zinazosimamia vinasaba katika mbegu za kiume za baba na tishu za titi la binti yake.

Kwa kawaida epijenetiki huwa ‘juu’ ya mpangilio wa DNA na huhifadhi urithi kutoka kizazi kimoja cha seli hadi kingine.

Kwa sababu ya sehemu hizo, aina tofauti za seli zilizokuzwa ndani ya mazingira aina moja zinaweza kuhifadhi tabia tofauti.

Kwa maneno mengine epijenetik ni mabadiliko ya kikemikali ya urithi ambayo yanaweza kuzima au kuwasha vinasaba fulani.

Huzidi kutambulika kama kifaa ambacho huruhusu athari za kiafya za mazingira au staili ya maisha kurithiwa vizazi vijavyo.

Hufanya kazi kwa kubadili protini, ambazo zinadhibiti DNA, kuongeza au kuondoa taswira ya kikemikali inayobadili muundo wa seli au kupitia molekuli za vinasaba.

Hivyo, unene huonekana wakati mwingine kurithiwa na familia kama ilivyo kwa saratani za titi na kina mama wanene wanaaminika kuchochea hali zote hizo mbili.

Wanawake wenye uzito mkubwa katika unene unaweza kuzalisha watoto wakubwa, ambao wanaweza kuongeza hatari ya saratani ya titi katika maisha ya baadaye ya watoto wao hao.

Tafiti nyingi zimejikita upande wa masuala ya uzazi, lakini ni chache zilizoangalia ushawishi wa baba mwenye uzito mkubwa au unene katika mustakabali wa wa siku za usoni wa afya ya watoto wake watakaozaliwa.

Utafiti huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Georgetown, Marekani ulitumia panya wa kimaabara lakini matokeo yanatumika kwa wanadamu pia.

Profesa Dk. Sonia de Assis aliyeshiriki utafiti huo anasema: ‘Utafiti huu unatoa ushahidi kuwa katika wanyama, uzito wa mwili wa akina baba wakati wa utungaji mimba huathiri uzito wa binti zao wakati wa uzazi na utotoni – pamoja na kuongeza hatari ya saratani ya titi katika maisha yao ya baadaye.

Suluhu alisema ni wanaume na wanawake kula vyakula bora, kuhakikisha miili yao ina afya na kudhibiti staili mbovu za maisha si tu kwa faida yao bali pia watoto wao watarajiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles