30.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

UHURU ATAKA RAILA ASTAAFISHWE SIASA

NAIROBI, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta amewataka wafuasi wake waliopo katika ngome zake muhimu, wajitokeze kwa wingi Agosti 8, ili mpinzani wake Raila Odinga astaafu siasa.

Akiwa katika ziara yake ya kuwinda kura katika kipindi hiki cha lala salama, zikiwa zimebaki siku 11 tu, Uhuru aliwaaambia wafuasi wake kuwa matokeo yataamuliwa kwa jinsi watakavyojitokeza kumpigia kura.

“Hali halisi ni kuwa mkijitokeza kwa wingi na mnipigie kura, basi huyu mtu wa kutusumbua kila uchao atakuwa amepata nauli ya kuelekea nyumbani kwake kustaafu siasa,” alisema Uhuru.

Akiwa katika Kaunti ya Murang’a, Rais Uhuru alisema: “Kile ambacho sitachoka kuwaambia ni kuwa kwa wakati huu nawahitaji kwa dhati. Kwa unyenyekevu nawapa tahadhari kuwa mkizembea na kura zenu, basi mambo yataishia kwa sisi kushindwa. Mkijitokeza kwa wingi, mambo yatakuwa murua kwetu.”

Aidha aliwaongoza wenyeji kuapa hadharani kuwa watajitokeza kwa wingi na si tu kupiga kura, bali ni kumpigia.

Alisema: “Ufanisi waja kwa kuwa hali ambayo tumekuwa tukifanya, ni kuandaa msingi wa kubeba miundombinu kadhaa ya upanuzi wa kiuchumi.”

Akitetea kutohudhuria mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa Jumatatu alisema: “Ratiba yangu ya kampeni na ambayo niliwasilisha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), haikuorodhesha mdahalo huo kama moja ya jukwaa langu la kampeni.”

Alisema kuwa hadi sasa haoni ni kwa nini kumezuka mjadala kuhusu kususia kwake mdahalo huo.

“Mjadala wa nini ilihali sioni manufaa gani nijitokeze katika ukumbi huo kujibizana na huyo mtu ambaye kila saa amejawa na uhasama na propaganda dhidi ya Serikali yangu?” alihoji.

Alisema kuwa kura haziko katika runinga na midahalo, bali ziko katika mikono ya Wakenya ambao haja yao ni kusaidiwa kujiinua kimaisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,358FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles