23.9 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

UHAMIAJI YASHIKILIA PASIPOTI YA MKURUGENZI TWAWEZA

|Bethsheba Wambura, Dar es SalaamMkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan  Eyakuze, amesema Idara ya Uhamiaji inashikilia hati yake ya kusafiria tangu Julai 24, ambapo pia licha ya kuwa na hati ya dharura, juzi Agosti Mosi mwaka huu alizuiliwa kusafiri kwenda jijini Nairobi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Agosti 3, Eyakuze amesema aliitwa uhamiaji na kutakiwa kupeleka hati yake ya kusafiria bila kuwa na taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hilo.

“Niliitwa Uhamiaji nikahojiwa kidogo na kuambiwa nipeleke pasipoti yangu sikuona haja ya kukataa sababu ni haki yao kuchukua, ila hadi sasa sijapata tamko rasmi kwa nini wamechukua,” amesema.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema Twaweza wataendele kufanya kazi zao kama kawaida pamoja na changamoto wanazopitia, ikiwamo kutumiwa barua mbili na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ikiwahoji kuhusu uhalali wa programu yao Sauti za Wananchi na kuwataka wafafanue kwanini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,298FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles