25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Uhaba wa maji Kibondo wananchi waililia Serikali

MWANDISHI WETU-Kibondo

WANANCHI wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, wameiomba Serikali ya Rais Dk. John Magufuli kuwasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa maji inayowakabili.

Wakizingumza leo mjini hapa, wananchi hao wamesema kero maji imekuwa kubwa kwao na kwamba wanaimani na Serikali Ikisikia kilio chao itatafuta
ufumbuzi ili waondokane na changamoto hiyo ambayo wamekuwa nayo kwa muda mrefu.

Akizungumza zaidi kuhusu changamoto ya kukosekana kwa maji ya kutosha Mkazi wa Station One, Ally Kasato amesema wanalazimika kufuata maji umbali wa wa zaidi ya kilometa mbili kutoka katikati ya maji yanayopatikana.

Amesema kuwa dumu moja la maji lenye ujazo wa lita 20 linauzwa Sh 700 kutokana na umbali wa kuyafuata maji hayo kwa kutumia usafiri wa baiskeli.

“Kilio chetu kikubwa hapa kwetu Kibondo ni uhaba wa maji, ni Kweli kuna changamoto nyingine makini hizo angalau kidogo tunao uwezo wa kuzitatua wenyewe lakini kwenye shida ya maji hili limetuzidi uwezo, hivyo Ombi letu Kwa Serikali itusaidie Ili tuwe na maji ya uhakika.

“Maji tunayotumia sasa ni ya Chemchem ambayo ni salama kwani yalipimwa na wataalamu na kisha wananchi tukaelezwa yapo Salama. Hivyo hata kama watafanya utaratibu wa kutuvutia maji kutoka yalipo yakaja mjini itatusaidia,”amesema.

Aidha ameshauri iwapo itawezekana Serikali ya Wilaya ya Kibondo kwa Kushirikiana na Serikali Kuu iwaruhusu wananchi kuchimba Visima vingine vya maji ili kupunguza msongamano wakati wa kuchota maji,”amesema.

Hata Hivyo amesema siku za karibuni walikuwa na kikao na viongozi wa Wilaya y Kibondo kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo ambapo walihakikishiwa na viongozi kuwa wataangalia uwezakano wa kutoa kibali chha kuchimbwa visima vingine viwili Ili kupunguza adha hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles