29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wakosa huduma za afya kwa miaka 58

Na Upendo Misha, Hai

WANANCHI zaidi ya 19,000 wa vijiji  vilivyopo katika Kata za mnadani, Weruweru na Masama Rundugai, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wamekosa huduma za afya kwa miaka 58 tangu nchi ilipopata uhuru.

Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa Kituo Cha Afya katika Kijiji Cha Longoi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, alisema kijiji hicho kimekuwa kikikabiliwa na ukosefu wa huduma za afya kwa miaka mingi.

Sabaya alisema wananchi kutoka katika maeneo hayo wamekuwa wakitembea zaidi ya kilomita 20 kwenda kutafuta huduma za afya katika maeneo jirani, hali ambayo imekuwa ikisabahisha vifo vya wanawake wajawazito na wagonjwa wengine.

“Maeneo haya ya tambarare yamekuwa yakionekana kama yametengwa na kubaguliwa huku maeneo ya juu milimani yakionekana kuwa na maendeleo ikiwemo kuwa na huduma zote muhimu za kijamii”alisema

“Baada ya kuona dhana hiyo iliyojengeka kwenu nilibuni namna ya kuwasaidia kwa kufanya jitihada za kutafuta fedha ili kujengwa kwa kituo hichi ambacho kinategemewa kuhudumia maelf ya wananchi wa maeneo haya ya tambarare”alisema

Akizungumza wakati akizindua ujenzi wa kituo hicho cha afya, Sabaya alisema kitagharimu zaidi ya Sh milioni 300, fedha ambazo zinatokana na michango ya vyama vya ushirika.

“Fedha hizi zimetolewa na vyama vya ushirika ambapo tuliwaomba katika bajeti yao mwaka 2018/19kutenga asilimia 50 kwaajili ya kuchangia ujenzi huu lakini pia bado wananchi mnapwaswa kushiriki kutoa mchango wenu wa nguvu kazi na fedha”alisema.

Mbali na hilo h alitoa onyo kwa wananchi kuacha wizi wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho na kwamba yeyote atakayebaika hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Akizungumzia ujenzi wa kituo hicho Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai, Irene Haule, alisema kituo hicho kitajengwa na kukamilika baada ya miezi mitatu na watatumia mafundi jamii ili kupunguza gharama za ujenzi.

“Kituo kitakuwa na majengo matatu ambayo ni jengo la wagonjwa wa nje, jengo la mama na mtoto na jengo la maabara na kitakamilika ndani ya miezi mitatu kwa kutumia fedha hizo”alisema.

Akizungumzia hali upatikanaji wa huduma za afya katika wilaya hiyo, alisema kunaupungu wa vituo vya afya kwa asilimia 65 na kwamba ujenzi huo itasaidia kupunguza tatizo hilo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Yohana Sintoo, aliwataka wananchi kulinda na kudhamini miundombinu itakayokuwepo katika kituo hicho ili iwe endelevu kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa bodi za vyama vya ushirika, Fredrick Urassa, alisema vyama vya ushirika vilikubali wito wa kuchangia ujenzi wa kituo hicho kutokana na ukweli kwamba awali vyama hivyo vilikuwa vikijikita katika kutoa maendeleo kwa jamii lakini dhana hiyo ilikufa baada ya ubadhirifu kushika kasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles