27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

UGAIDI WAHUSISHWA NA GHASIA ZA ISRAEL

TEL AVIV, ISRAEL


JESHI la Israel limerusha video fupi inayomwonyesha mwanachama mwandamizi wa Hamas, akisema Wapalestina 50 waliouawa na Israel katika Ukanda wa Gaza mwanzoni mwa wiki hii, walikuwa wanamgambo wajiitao Dola la Kiislamu (IS).

Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Ofir Gendelman, alisema ni ushahidi kuwa hayakuwa maandamano ya amani bali harakati za kundi la Hamas.

Kwa mujibu wa Gendelman, Israel itawasilisha mara moja video hiyo kama ushahidi kwa jumuiya ya kimataifa kuwa maandamano hayo yalikuwa ni mwamvuli uliogubika ugaidi.

Israel imekabiliwa na upinzani mkubwa wa kimataifa juu ya mwenendo wa askari wake mwanzoni mwa wiki hii, huku nchi kadhaa zikitaka uchunguzi huru na wa haki baada ya Wapalestina zaidi ya 60 kuuawa.

Wapalestina hao waliuawa mapema wakati wakiandamana katika kumbukumbu ya miaka 70 ya kunyang’anywa kwa ardhi yao na Israel pamoja na kupinga kitendo cha Marekani kuhamishia ubalozi wake katika mji unaoogombaniwa wa Jerusalem.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles