27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Ufuatiliaji na Tathmini haviepukiki katika utekelezaji wa miradi na mipango ya maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Arusha

IMEELEZWA kuwa suala la Ufuatiliaji na Tathmini lina umuhimu mkubwa katika kuangalia utekelezaji wa Mipango kuanzia ngazi ya mamlaka za chini hadi ngazi ya taifa katika utendaji hususan kwenye miradi, ikilinganishwa na namna gani inakwenda sawasawa au inatekelezwa kama ilivyopangwa.

Hayo yameelezwa leo Septemba 13, 2023 jijini Arusha na Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Cosmas Ngangaji katika siku ya pili ya Kongamano la Pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea jijini humo ambapo amesema kuwa suala Ufuatiliaji na Tathmini linajikita zaidi katika vitendea kazi vinavyotakiwa kutumika pamoja na michakato inayotumika kama inafanya kazi na kuleta matokeo chanya hususan katika sekta ya umma.

Washiriki wakifuatilia uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa siku ya pili ya Kongamano la pili la Wiki ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea Jijini Arusha.

Akitolea mfano wa dhana ya tathmini ya utoaji wa huduma za kijamii, Bw. Ngangaji alisema kuwa, miradi mingi ya Serikali inatakiwa kuwekewa misingi endelevu ili wananchi waweze kupata huduma sahihi na kwa wakati.

Akiongea katika kongamano hilo Bw. Mussa Mshirazi Mbarouk kutoka Tume ya Mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar alisema, suala la Ufuatilijai na Tathmini ni suala linalohitaji kujifunza mara kwa mara ili kusaidia kujenga uwezo katika utendaji wa shughuli za kila siku.

Kongamano la Pili la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji na Tathmini linaloendelea Jijini Arusha limeingia katika siku ya pili ambapo mada mbalimbali zimeendelea kuwasilishwa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uelewa wa Tathmini, majadiliano bayana juu ya matokeo halisi na mbinu muhimu za kuleta mbadiliko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles