27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kampeni ya Tutunzane Mvomero kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji

Na Ashura Kazinja, Morogoro

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro inatarajia kuzindua Kampeni ya ‘Tutunzane’ ambayo imelenga kuwaleta pamoja wafugaji na wakulima ili waweze kushirikiana katika shughuli za kilimo na ufugaji.

Wakulima na wafugaji wakiwa katika kikao cha mipango kuelekea katika uzinduzi wa jujwaa la Tutunzane na mkuu wa wilaya ya Mvomero (hayupo pichani).

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Septemba 13, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, amesema kampeni hiyo ya kihistoria ya mwaka huu itakuwa endelevu kwa kila mwaka na imelenga kuondoa tofauti zilizopo kati ya wakulima na wafugaji kwa kuanzisha mashamba ya malisho ya mifugo pamoja na uchimbaji wa marambo (mabwawa) ya kunyweshea mifugo pamoja na kilimo cha zao la ufuta kama zao la mkakati kiwilaya.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero Judith Nguli (kushoto) akizungumza na wakulima na wafugaji.

Amesema kampeni hiyo pia itasaidia utunzaji wa mazingira, kwa pande zote mbili kati ya  wafugaji na wakulima na kwamba itaifanya Mvomero kuwa ya kipekee na yenye sura nyingine tofauti na ya awali ya changamoto za kimazingira na migogoro,mbalimbali.

“Sasa hii kampeni ya Tutunzane Mvomero ukiliangalia neno lenyewe Tutunzane maana yake nitunze nikutunze, nilee nikulee, ndio maana ya kampeni yangu, nikampeni endelevu na inalenga makundi hayo ya wakulima na wafugaji katika mlolongo wa kuangalia mazingira, tunaona mazingira yetu kwa sasa ambayo ndio ajenda kuu ya dunia na mnaona tunapitia mabadiliko ya tabia nchi kwa sana hata imeweza kubadilisha misimu,” amesema Nguli.

“Kwa hiyo tumeamua kumshirikisha mfugaji katika zana hiyo ya Tutunzane, maana yake mfugaji amtunze mkulima lakini mfugaji atunze mazingira na vyanzo vya maji,kwanini mfugaji amtunze mkulima?maana yake mfugaji akifuga ufugaji ulio sahihi na wa kisasa ambao hauleti madhara kwa mkulima maana yake mfugaji atakuwa amemtunza mkulima,” amesisitiza Nguli.

Pia, amesema mkulima anatakiwa kumtunza mfugaji kwa kufanya kilimo chake vizuri bila kuhamahama na kuacha kulima kwenye mita sitini kwenye mito, hapo atakuwa na uwezo wa kutunza mazingira na vyanzo vya maji, na kuacha kukata kata miti ovyo, hivyo atakuwa amemtunza mfugaji kwani atapata chakula vizuri na maji ya kutosha.

Aidha, amesema kabla ya kuanza kwa kampeni hiyo wanataraji kuzindua jukwaa la Tutunzane Mvomero ambalo litakuwa na wadau mbalimbali na linatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 4 mwaka huu.

“Lakini katika hili tutakwenda kuzindua jukwaa, sasa hiki kikao cha leo ni cha mipango kuelekea uzinduzi wa jukwaa, jukwaa hili la Tutunzane Mvomero litakuwa na wadau ambao tumeshawaita,” amesema Nguli.

Kwa upande wake,kiongozi wa Jumuiya ya Wakulima wilaya ya Mvomero kutoka Kijiji cha Mkindo, Mganga Kazumba, amempongeza mkuu wa wilaya ya Mvomero kwa kuanzisha kampeni hiyo, kwani itawasaidia tofauti na awali ambapo walikuwa hawakutanishwi inapotokea migogoro wala kuwa na ukaribu wa wazi kati ya wakulima na wafugaji.

“Tupo hapa kwa ajili ya kampeni ya Tutunzane,kwamimi naona kama sehemu muhimu, kwa maana gani? hatua zilizochukuliwa na wilaya kutuita na kutuweka pamoja wakulima na wafugaji tunaweza kueleza changamoto za mkulima zikasikika na za mfugaji zikasikika na mwisho wa siku tukajadiliana namna gani tufanye,hivyo kwa kampeni hii ya tutunzane, mimi naamini tanaweza kufaulu,”amesema Kazumba.

Naye Mfugaji, Longido Shambakubwa ambae ni mkazi wa kijiji cha Dakawa Sokoine amewahimiza wafugaji wenzake kuona umuhimu wa kuwa na mashamba ya malisho na kufuga kisasa ili kuweza kupata mifugo yenye bei nzuri na wanaokamuliwa kutoa maziwa mengi na ya kutosha.

“Zoezi la upandaji wa malisho katika maeneo ya wafugaji ni jambo jema ambalo linaweza kuchochea swala la ufugaji na kupunguza migogoro ya hapa na pale, mifugo yetu ikipata malisho mazuri bila shaka wafugaji watapata manufaa mazuri na kunufaika kwa namna moja au nyingine ikiwemo ya kuwa na makazi bora na ya kudumu.

“Baada ya kupata mafunzo nikaja nikauza baadhi ya mifugo yangu nikanunua mashamba,nikaanza kufuga kisasa kwa maana ng’ombe wangu wakawa hawatoki nje ya eneo langu, pia nikawahamasisha wafugaji wenzangu kupitia nafasi niliyokuwa nayo kuwa waje kujifunza namna ya kupanda malisho na wengi walikuja kutoka sehemu mbalimbali,” amesema Longido.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles