29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Tundu Lissu aonywa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Tundu Lissu ameonywa kuacha kuwagawa Watanzania kwa kufanya siasa za uchonganishi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Team Wazalendo, Frank Rugwana(Katikati) akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.

Onyo hilo limetolewa leo Septemba 13, 2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Team Wazalendo, Frank Rugwana, ambapo amesema kuwa wanakemea wanasiasa na wanaharakati ambao wanafanya uchochezi kwa kuzungumza mambo ya uongo kwa lengo la kuvunja Amani na utulivu ulipo kama taifa moja.

“Tunawataka akina Lissu (Tundu Lissu) na makundi yake waache kuwachochea Watanzania ili washindwe kuwa wamoja. Zipo njia sahihi za kuwahamasisha Watanzania wakubali kuwaunga mkono kwenye chama chao pasipokutumia njia ya kuamsha hasira ili washindwe kuelewana na Serikali yao.

“Na hivi karibuni tutakwenda kuwaweka hadharani wale wote wanaofadhili na kushirikiana nao katika dhamira yao ovu ya kuvunja Amani ya taifa letu. Tutaanika mipango yao na baadhi ya vikao vyao wanavyofanya vyenye nia ovu ya kutugawa Watanzania,” amesema Rugwana.

Amesema wao hawamchukii Mwanasiasa huyo badala yake hawakubaliani na baadhi ya matamshi ambayo amekuwa akiyatoa kwenye majukwaa ya siasa kwa siku za karibuni.

“Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ametoa fursa ya vyama vya siasa kufanya mikutano, hivyo haikubaliki kuwapo na baadhi ya wanasiasa wachache ambao wamekuwa wakifanya siasa za chuki.

“Hivyo, tunatoa rai kwa niaba ya Watanzania wazalendo tunamsihi Lissu na makundi yake yote kuacha mara moja kutugawa Watanzania wachache kwa kuchochea chuki dhidi ya Rais Samia na Serikali yake kwa maslahi yao.

“Waheshimu na kutumia jukwaa hili la uhuru wa kisiasa uliopo kistaarabu badala ya kupandikiza chuki,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema kuwa wao wako tayari kushirikiana na Lissu iwapo atayafanya siasa za kiungwana zinazojenga na kuwaleta Watanzania pamoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles