31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Twaha Kiduku awaita mashabiki kuona akimchakaza Mganda Des 26

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuona jinsi atakavyomchapa Mganda, Mohammed Sebyala katika pambano la Usiku wa Mabingwa.

Pambano hilo litakalosindikizwa na mapambano mengine mengi ya uzito tofauti, litafanyika Desemba 26, 2023, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Akizungumza wakati mabondia hao wakitamba mbele ya waandishi wa habari leo Desemba 24,2023, Kebbys Hoteli Dar es Salaam,Kiduku amesema amemtazama mpinzani wake yuko vizuri kalini yeye amejiandaa kutoa burudani kwa watanzania.

“Nimemuangalia ni bondia mzuri lakini naamini siwezi kuwaangusha watanzania, naomba dua zenu, bila shaka nitawapa burudani nzuri siku hiyo, napanda ukingoni kama nyoka aliyekanyagwa mkia,” amesema Kiduku.

Naye Sebyala ametamba kumfundisha ngumi Kiduku kwa kuwa hatua aliyofikia yeye ni mwalimu wa mchezo huo sasa.

Katika pambano lingine kubwa Oscar Richard amejinadi kumpiga mpinzani wake kutoka Afrika Kusini, Sabelo Ngebinyana, akitamba kuwa asimchukulie poa.

” Nahisi kama amekuja kwa kukariri na mimi namwambia asije kwa kukariri, kikubwa kuheshimiana. Nimeona hata mahojiano yake amekiri kuwa mimi ni mzuri,” ametamba Oscar.

Kwa upande wa wanawake Sara Alex na Jesca Mfinanga Kila mmoja ameonekana kupania kumchapa mwenza hasa baada ya kutaka kupigana wakati wa utambulisho.

Akizungumzia maandalizi yao, Mratibu wa pambano hilo kutoka Peaktime Sports Agency, Bakari Khatibu, amesema maandalizi yamekamilika kwani tiketi za mzunguko tayari zimekwisha bado za VIP.

Amesema burudani itakuwa ya kutosha na kuwataka mabondia kuonesha mchezo safi kwa kupigana ngumi na si kukumbatiana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles