27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya haki za binadamu yapongeza wafungwa kuachiwa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, imepongeza uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli kutoa msamaha wa wafungwa 5,533.

Rais Dk. Magufuli alitoa msamaha huo, wakati akihutubia wananchi Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza Desemba 9, mwaka huu wakati wa sherehe za miaka 57 ya Uhuru.

Taraifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa tume hiyo,  Jaji mstaafu, Mathew Mwaimu, ilisema uamuzi huo ni wa kipekee tangu Tanzania ipate uhuru kutokana na idadi kubwa ya wafungwa kusamehewa.

“Tume inachukulia uamuzi  wa rais  kama jambo ambalo linaweka nguvu na mkazo sehemu ya majukumu yake ya kuhakikisha  haki za binadamu zinafurahiwa na watu wote, ikiwamo wale walio magerezani. 

“Tume imefurahishwa na kauli aliyoitoa rais katika maadhimisho hayo kuhusu kusikitishwa kwake na hali ya magereza, kauli hii inaonesha dhamira ya dhati aliyonayo binafsi na Serikali yake kulinda na kuhifadhi haki za wafungwa na mahabusu katika magereza,”alisema taarifa hiyo.

Tarifa hiyo, ilisema moja ya jukumu la tume kwa mujibu wa ibara 130 (1) ya Katiba kifungu cha 6 (1) cha sheria ya tume, ni kutembelea magereza ili kuangalia uhifadhi wa haki za binadamu  sehemu hizo na kutoa mapendekezo yanayofaa kuimarisha na kuboresha mazingira ya magereza.

Ilisema tume imekuwa ikifanya ziara za mara kwa mara  magereza mbalimbali kwa lengo la kutekeleza jukumu hilo. 

“Tume imekuwa ikigundua changamoto kadhaa zinazowakabili wafungwa na mahabusu, zikiwamo mlundikano wa wafungwa na mahabusu, kesi zao kuchukua muda mrefu kumalizika. Tume imekuwa ikitoa mapendekezo kwa taasisi husika kurekebisha hali hiyo,”alisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, iliongeza kuwa taasisi zenye dhamana ya kuhifadhi wafungwa na mahabusu, zitaongeza kasikulinda na kuhifadhi haki za makundi hayo.

“Kauli hii, itazifanya taasisi zenye dhamana ya upelelezi kufanya kazi haraka ili kupunguza muda wa mahabusu kukaa magerezani muda mrefu. “Mahakama na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka  hazina budi kuongeza juhudi kusikiliza na kumaliza kesi za jinai haraka ili kupunguza muda wa mahabusu kukaa magerezani,”ilisema taarifa hiyo .

Tume hiyo, imetoa ushauri wafungwa wote walionufaika, watumie mafunzo waliyoyapata wakiwa gerezani kushirikiana na Watanzania wenzao kuisaidia kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles