25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Hatujapokea barua rasmi ushiki wa Kenya Kili Marathon-Bayo

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mkurugenzi wa mbio za Kili Marathon, John Bayo, amesema bado hawajapokea barua rasmi kutoka nchini Kenya inayoelezea kusitisha wanaridha kutoka nchini humo kushiriki mbio hizo.

Bayo ameyasema hayo leo Alhamis Februari 25,2021 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewaeleza maandalizi yanaendelea vizuri.

Mkurugenzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon

Amesema kuwa kuna uvumi unaendelea katika mitandano ya kijamii ambayo hawawezi kuiamini hadi watakapotutumia barua rasmi, na kwamba maandaalizi yamefikia asilimia 95 ikiwemo njia za kukimbilia.

“Nimewasiliana na Mkurugenzi wa michezo nchini kwetu nimemwelezea juu ya Wakenya kutoshiriki mbio hizo na kuagiza tusubiri barua rasmi kutoka nchini Kenya,” amesema Bayo.

Mkurugenzi Mtendaji wa hoteli ya Keys ya mjini Moshi, Lucy Owenya, amesema kuwa maandalizi ya mbio yanafanyika katika hoteli hiyo kwa washiriki wambioza km 5, 21 na km 42.

Amesema kwa wakimbiaji wa mbio za km 21 nafasi zimeshajaa ambapo washiriki zaidi ya 5000 wamejitokeza kushiriki mbio hizo huku washiriki wa mbio za km 5 na km 42 bado wanaendelea kujiandikisha katika hotel ya key’s.

Lucy amesema maandalizi yanaendelea vizuri huku wakichukua taadhari kubwa ya kujikinga na maambikizi ya virusi vya corona19 na kutoa wito kwa washiriki na wananchi kwa ujumla kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kupitia wizara ya afya.

Mashindano ya mbio za Kill Marathoni mwaka huu yamekuwa tofauti na miaka mingine kutokana na maambikizi ya virusi vya ugonjwa corona ambapo wanariadhara kutoka  nchini Kenya wameshatangaza kutoshiriki mbio hizo.

Amesema kutokana na hali hiyo athari zimekuwa ni kubwa kibiashara kutokana na washiriki hao kusitisha kuja kushiriki mbio hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles