Tuhuma za Nagu kuiba kura zazua taharuki

0
986

Dr.MaryNaguNA MWANDISHI WETU.

TAARIFA ambazo zimetajwa kuwa ni za kizushi dhidi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Uhusiano, Dk. Mary Nagu kwamba amekamatwa na masanduku kumi yakiwa kura zilizokwisha pigwa zimezua taharuki katika jamii.

Habari hiyo ya Nagu, iliyoanza kusambaa kwa kasi jana jioni kupitia mitandao ya kijamii muda mfupi kabla ya gazeti hili halijakwenda mitamboni iliibua mshtuko na mshangao kwa jamii hususani watu wanaofuatilia mwenendo wa Uchaguzi Mkuu kwa ukaribu.

Gazeti hili lilimtafuta Dk. Nagu kwa njia ya simu lakini iliita bila kupokelewa.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, alikanusha habari hizo akisema hazina ukweli wowote.

“Wanaosambaza habari ni wajinga kwa sababu Dk. Mary Nagu hadi jioni alikuwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara pamoja na wapambe wake wa  Chama Cha Mapinduzi na wala hajahusika na jambo lolote linalohusiana na tuhuma hizo” alisema Kamanda huyo wa Polisi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here