24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL yachochea mageuzi ya ‘Tiba Mtandao’

*Mkurugenzi JKCI asema amerahisisha huduma na kuokoa muda

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Ukuaji wa Teknolojia nchini umesaidia kurahisisha utendaji kazi kwa taasisi mbalimbali na kupunguza muda wa utoaji huduma kwa jamii.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Peter Kisenge, alipotembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) katika maonyesho ya 47 ya Biashara(Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo amesema uwepo wa Teknolojia hiyo kumerahisisha huduma kwani wanaweza kuongea na mgonjwa popote anapokuwa na tatizo na kumsaidia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Peter Kisenge, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) katika maonyesho ya 47 ya Biashara(Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam Juni 2, 2023.

Amesema TTCL imefunga mtandao wa “Internet” unaofahamika kama Tiba Mtandao katika hospitali zote nchini na kwamba imefanya kumfikia mgonjwa kwa wakati na kumsaidia.

“Hii huduma imetusaidia sana madaktari kwani tunaweza kuwasiliana na mgonjwa na kuongea naye huku unamuona hata kama anakipele una kiona na akisema maumivu unakuwa unamuona unajua jinsi ya kumsaidia,” amesema Dk. Kisenge.

Naye, Afisa Mwandamizi Shirika la Mawasilino Tanzania (TTCL), John Yahaya amesema mpango wa uimarishaji wa mifumo ya internet yenye kasi ya juu katika mfumo wa tiba mtandao umelenga kuboresha huduma.

Amesema, hatua hiyo inamuwezesha daktari kuhudumia mgonjwa kutoka sehemu moja hadi nyingine bila changamoto yoyote.

“Mbali na kupunguza msongamano katika upatikanaji wa huduma inaunganisha watu kutoka maeneo mbalimbali, kwa sasa mgonjwa aliyekuwa hapa Dar es Salaam anaweza kutibiwa na daktari aliyopo Mtwara kupitia mfumo wa tiba mtandao kwa njia ya video ikiwa na kasi ya hali ya juu,” amesema Yahaya.

Ameeleza kuwa, maboresho hayo ya huduma za internet ndani ya TTCL yamelenga kuwezesha wateja kupata huduma kwa unafuu na uhakika hadi majumbani na kuwasiliana bila kikwazo ikiwemo cha kukatikatika kwa mawasiliano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles