25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

Kuimarika kwa Teknolojia kumeiongeza ufanisi- TRA

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Ukuaji wa Teknolojia nchini umesaidia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya mapato na kulinda afya ya mtumiaji wa bidhaa mbalimbali kwa kuweka stemp kwenye kila bidhaa.

Akizungumza Julai 2, na Waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya 47 ya biasharaa ya Sabasaba, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kuhakiki bidhaa zao kabla ya kuzitumia ili kulinda afya zao.

Aidha, Kayombo ametoa wito kwa wananchi kutembelea kwenye banda lao ili kupata elimu zaidi kuhusu uhakiki wa bidhaa.

“Sasa hivi kila mtu anatumia simu janja hivyo ni rahisi kutumia teknolojia hii kuhakikisha mapato hayapotei lakini afya za wananchi zinaimarika kwa kutotumia bidhaa zisizo na ubora,” amesema Kayombo.

Amesema uwepo wa mfumo huo umesaidia kuondosha bidhaa bandia sokoni na kusababisha mapato kuongezeka.

Naye Mtaalam wa Mfumo huo (ICT TECHNICAL II), Nyakina Mafuru amesema Kwa kutumia stemp kutasaidia mtumiaji bidhaa hiyo kujua imetengenezwa wapi na ukomo wake wa matumizi na pia kujua kama imethibitishwa na mamlaka husika ikiwemo TBS.

“Matumizi ya stemp ya kielektroniki yameiondoa ile stemp ya karatasi iliyokua ikitumika zamani kwani imeonekana kutokuwa bora na badala yake wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakitengeneza stika bandia na kuzitumia kwenye bidhaa zao hatua inayosababisha kukwepa kodi,” amesema Marufu.

Ameongeza kuwa mfumo huo ni mzuri na unaisaidia TRA kujua kodi halali kwa bidhaa lakini pia mfanyabiashara atajua amezalisha kiasi gani huku mtumiaji wa mwisho wa bidhaa hiyo akiona uhalali wake na kwamba itasaidia kulinda afya.

Amesema ili kuhakiki bidhaa mtumiaji anapaswa kupakua application iliyopo kwenye simu janja.

TRA imewataka kila mlipa kodi nchini kujilinda mwenyewe kwa kulinda afya yake ambapo kampeni hiyo ya kuhamasisha uhakiki wa bidhaa kielektroniki imekuja na kauli mbiu isemayo “Linda afya hakiki stempu kwenye kinywaji chako mwenyewe”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles