25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

TAWA: Wekezeni kwenye maeneo ya wanyamapori

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watanzania, wawekezaji na wageni kutoka Mataifa mbalimbali wametakiwa kuwekeza katika maeneo ya Wanyamapori kwa kuwa kuna fursa nyingi za uwekezaji.

Akizungumza leo Julai 2, jijini Dar es Salaam wageni waliotembelea banda la hilo la maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya Kibiashara Afisa Mhifadhi Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA ), Gregory Kalokole amesema TAWA ina fursa za uwekezaji unaotoa mwanya kwa wawekezaji wa aina mbalimbali kuwekeza katika sekta hiyo

Amesema yapo maeneo mengi yanayohitaji wawekezaji na uwekezaji katika taasisi hiyo kama vile maeneo ya utalii wa picha kwenye maeneo ya hifadhi za Wanyamapori, maeneo ya kihistoria yenye Utalii wa kiutamaduni, eneo la uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas – SWICA), Uwindaji wa Kitalii na Ufugaji wa Wanyamapori

“TAWA imetenga maeneo kadhaa Kwa ajili ya kufanyika shughuli za utalii wa picha kutokana na ikolojia na aina ya vivutio vilivyopo katika maeneo hayo ikiwemo Pori la Akiba Mpanga/Kipengere eneo ambalo lina maporomoko ya maji zaidi ya 10 ambayo hutoa burudani safi Kwa watalii.

“Mapori mengine ya Akiba ni Pande, Wamimbiki, Swagaswaga na Kijereshi ambapo wananchi wanakaribishwa kuwekeza kwenye miundombinu ya Utalii ikiwemo kujenga Kambi za Kulala wageni, hosteli, loji na maeneo ya mapumziko mafupi (Picnic Sites),” amesema Kalokole.

Naye, Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi Wote kutembelea banda la TAWA Ili kupata maelezo ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi hiyo.

“Hii ni fursa adhimu Kwa wawekezaji wote kutembelea banda letu ili waweze kupata ufafanuzi wa fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi yetu kwani TAWA ni sehemu sahihi Kwa uwekezaji na wawekezaji,” amesema Maganja.

Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu “Tanzania ni Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji” yameanza 28 Juni, mwaka huu na yanatarajiwa kufikia tamati Julai 13, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles