23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tshisekedi kunadi sera zake Kinshasa

KINSHASA, Congo DRC



UKIWA umebaki muda usiozidi mwezi mmoja  kabla ya uchaguzi mkuu uliosubiriwa kwa muda mrefu nchini hapa, kiongozi mkuu wa upinzani, Felix Tshisekedi anatarajiwa kurejea  mjini   kuzindua kampeni zake akigombea nafasi ya urais.

Felix Tshisekedi ni mtoto wa Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mwaka jana baada ya kutumikia miongo kadhaa katika kambi ya upinzani nchini.

Felix  ataingia kwenye kinyang’anyiro cha urais na mwenzake, Vital Kamerhe kama mgombea mwenza.

Habari zilizopatikana mjini hapa zinaeleza kwamba Feilix na  Kamerhe, wa chama cha UNC,  wanatarajiwa kuzindua kampeni zao kwa pamoja, baada ya makubaliano ya kuunganisha nguvu hali ambayo wengi wanaitazama kuwa italeta mgawanyiko   wa kura  za wapinzania  katika uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni   miezi minne tangu vyama vya upinzani vikubaliane   kusimamisha mgombea mmoja ambako Mbunge aliyekuwa hajulikani na wengi, Martin Fayulu, aliteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa niaba ya muungano wa vyama vyote.

Hata hivyo muda mfupi baada ya makubaliano hayo,  vyama vya UDPS na UNC vilijitoa kwenye muungano huo.

Tshisekedi sasa atawania nafasi ya urais kwa makubaliano kwamba Kamerhe atakuwa waziri mkuu wake .

Mpaka sasa ni wagombea 19  wanaowania nafasi moja ya urais  akiwamo mgombea wa chama tawala, Emmanuel Ramazani Shadary.

Taarifa zilizopo nchini hapa na za kutoka kwa mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Mbelechi Msochi, zinasema  vyama vya upinzani vinalalamika kutokuwa na fedha  za kuendesha kampeni zao.

Kwa sababu hiyo vinajibana  na fedha ndogo vilivyo nayo mpaka wiki mbili kabla ya uchaguzi ndipo vitakapoingia mchuano wa  kunadi sera zao kabla ya kuingia kwenye uchaguzi.

Uchaguzi huo ambao umecheleweshwa kwa miaka miwili  sasa unatarajiwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles