30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji amdhamini ‘Amber Ruty

KULWA MZEE – DAR ES SALAA



MCHUNGAJI wa Kanisa la Pentekoste la Emaus Bible, Daudi Mashimo na wenzake watatu wamewanusuru kukaa gerezani Mcheza Video, Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Ruty’ na Said Bakary Mtopal.

Mchungaji huyo aliwanusuru jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Washtakiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mchungaji Mashimo na Francis George walimdhamini Saidi Bakari, wakati Salma Omari na Asha Seif walimdhamini Amber Ruth.
Washtakiwa hao wameachiwa kwa dhamana jana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili, wenye vitambulisho vya Taifa na wamesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 15.

Washtakiwa hao na mwenzao, James Delicious aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana Novemba 2 mwaka huu walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Awali Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai katika kosa la kwanza washtakiwa wanadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile linalomkabili Amber Ruty.

Inadaiwa ametenda kosa hilo kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary Mtopali kumwingilia kinyume na maumbile.

Shtaka jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary Mtopali ambapo anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruty kinyume na maumbile.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya Oktoba 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambapo wanadaiwa kati Oktoba 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp.

Washtakiwa walipewa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 kila mmoja na kusaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 15.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles