31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Trump adai kuchoshwa kuandamwa New York, akacha makazi yake, akimbilia Florida

WASHINGTON, MAREKANI RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema atafanya makazi yake ya Palm Beach, Florida, kuwa ya kudumu baada ya kuondoka White House,  kuliko kurejea Trump Tower, huko New York.

Trump alisema hayo kupitia andiko lake la kwenye tweeter alilolitoa Alhamisi wiki hii wakati akiipongeza New York. Lakini aliongeza kuwa “pamoja na ukweli kwamba ninalipa mamilioni ya dola katika jiji hilo, serikalini na kodi nyingine za ndani kila mwaka, nimekuwa nikitendewa vibaya na viongozi wote wa kisiasa na jiji.”

Jarida la The New York Times awali Alhamis wiki hii liliripoti kuwa Trump amewasilisha hati ya kiapo kuhusu kusudio hilo  la kufanya Mar-a-Lago resort Florida kuwa makazi yake ya kudumu.

Trump, ambaye alizaliwa New York, alisema ” eneo hilo litakuwa mahali maalumu  moyoni mwake.

Wakati huo huo, uchunguzi unaofanywa na baraza la wawakilishi la Marekani kuhusu kumfungulia mashtaka Trump unawaangazia mawakili wawili wa Ikulu ya White kutokana na mazungumzo ya faragha juu kuondoa ujumbe unaoelezea kuhusu mawasiliano ya simu kati ya rais huyo na mwenzake wa Ukraine katika mfumo wa kompyuta wenye udhibiti mkali, ambao kwa kawaida hutumiwa kuhifadhi taarifa za siri kubwa.

Wachunguzi katika mchakato huo unaolenga kumfungulia mashtaka Trump, wamemtaka aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa taifa, John Bolton kutoa ushahidi wiki ijayo.

Lakini pia wanataka ushahidi wa watu wawili walioteuliwa kisiasa; John Eisenberg, wakili anayeongoza katika baraza la kitaifa la usalama na Michael Ellis, wakili mkuu mshirika wa rais.

Jopo hilo linachunguza mawasiliano ya simu ambapo rais Trump alimtaka rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kumfanyia hisani ya usaidizi wa kisiasa tarehe 25 mwezi Juni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles