
NAIROBI, KENYA
MKALI wa RnB kutoka Marekani, Trey Songz anatarajiwa kuungana na wasanii wengine wa Afrika ambao watashiriki kwenye msimu wa 4 wa Coke Studio Africa.
Taarifa za mkali huyo zilitangazwa na waendeshaji wa tamasha hilo kupitia ukurasa wao wa Instagram wiki hii, ambapo atakuwa msanii wa tatu kutoka Marekani kushiriki kwenye Coke Studio Africa baada ya Wyclef Jean na Ne-Yo.
Trey Songz atafanya kolabo na rapa wa Afrika Kusini ‘Emtee‘ ambayo itatiwa mikono na Dj Maphorisa.
Msimu huu, Tanzania itawakilishwa na Vanessa Mdee, Joh Makini na Yamoto Band huku Diamond akishiriki ile ya Afrika Kusini.