23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yawataka mawakala wa forodha kujiepusha na biashara za magendo

Mwandishi Wetu, Mbeya

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewataka mawakala wa forodha wanaofanya shughuli zao katika mipaka ya nchi kujiepusha na biashara za magendo kwani zina madhara kiuchumi, kijamii na kiafya.

Akizungumza wakati wa semina kwa mawakala wa forodha wanaofanya shughuli zao katika mpaka wa Tanzania na Malawi uliopo Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Diana Masalla amewasisitiza mawakala kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiforodha na wajiepushe kuwa sehemu ya wakwepa kodi.

Semina hiyo ni sehemu ya kampeni maalumu ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea kutolewa na TRA mkoani Mbeya kuanzia Mach 9 hadi 14, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Masalla, baadhi ya madhara ya kiuchumi ni pamoja na nchi kukosa mapato, kuua viwanda vya ndani kwa kuingiza bidhaa zenye viwango hafifu na kudidimiza uchumi wa nchi endapo bidhaa hizo zitapita njia zisizo rasmi na kutolipiwa ushuru wa bidhaa.

“Kwa upande wa madhara ya kiafya ni pamoja na kuingiza bidhaa ambazo hazijathibitishwa usalama wake na hivyo huenda zikasababisha mlipuko wa magonjwa kwa watakaozitumia.

“Ni hatari sana kuingiza bidhaa hasa za vyakula, pembejeo au viuatilifu ambavyo havijapimwa na kuthibitishwa na mamlaka husika za serikali, kwa hiyo mawakala wa forodha msije mkashiriki biashara za magendo msije mkaangamiza jamii”, amesema Masalla.

Pamoja na mambo mengine, amesema madhara ya kijamii ambayo yanayoweza kutokea kwa jamii ni pamoja na kuhatarisha usalama wa nchi na raia wake kwa kuingiza bidhaa zenye sumu na kuathiri jamii kwa kiwango kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles