Wizara ya Afya: Mloganzila si karantini wagonjwa wa corona

0
1260

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema Hospitali ya Mloganzila haijatengwa kuwa karantini ya wagonjwa watakaobainika kuwa na virusi vya corona na kwamba hadi sasa nchini hakuna mgonjwa wa virusi hivyo.

Akizungumza na Mtanzania Digital, kuhusu ujumbe uliosambaa mitandaoni kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameiteua hospitali hiyo kuwa karantini ya wagonjwa hao, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Serikali wa wizara hiyo, Idara Kuu ya Afya, Gerald Chami, amesema ni uzushi.

“Hakuna kitu kama hicho. Hakuna mgonjwa wa corona si Mloganzila tu bali nchini kwa ujumla.

“Waziri amezungumzia kuhusu corona kuwa watu wawe na ufahamu na wachukue tahadhari, lakini hajazungumzia Mloganzila wala wagonjwa wawili wa corona kama inavyosemekana.

“Amezungumzia kuwa kila halmashauri itenge maeneo kwa ajili hiyo kama tahadhari ikitokea kuna tatizo kama hilo, ingawa hadi sasa hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona nchini,” amesema Chami.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here