30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

TRA YASAINI MKATABA WA MAFUNZO NA ZRB

Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) yatakayowezesha wafanyakazi wa bodi hiyo kujengewa uwezo.

Mkataba huo umesainiwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Alphayo Kidata kwa niaba ya Chuo cha Kodi (ITA) pamoja na Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Kidata alisema kuna jumla ya kozi 64 zitafundishwa katika chuo hicho kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea maarifa wafanyakazi hao ili waweze kuimarisha utendaji wao.

“Kazi ya kukusanya mapato na kodi mbalimbali inahitaji elimu ya mara kwa mara hivyo ni mategemeo yetu kwamba baada ya mafunzo hayo wenzetu wa Bodi ya Mapato Zanzibar wataweza kuimarisha utendaji kazi wao hivyo kupanua wigo wa ukusanyaji mapato ya Serikali,”alisema Kidata.

Alisema makubaliano hayo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi hivyo zoezi hilo litaanza mnamo mwezi Machi hadi Juni mwaka huu.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar, Amour Bakari, alisema taasisi za ukusanyaji wa fedha zimepewa jukumu la kukusanya mapato ya Serikali hivyo ni lazima watumishi wa taasisi hizo wawe makini na kwenda na teknolojia ili kurahisisha mchakato wa ulipaji wa kodi.

“Tunatarajia  matokeo ya makubaliano haya katika kipindi kifupi kijacho kwani tayari maandalizi ya kozi ya kwanza yamekamilika na mnamo Machi 13 baadhi ya watendaji watashiriki katika mafunzo ya mwanzo yatakayoendeshwa na chuo hicho,” alisema Bakari.

Taasisi hizo zitahakikisha zinatengeneza misingi imara itakayoweza kusaidia kuinua mchakato mzima wa ukusanyaji wa kodi kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kuwajengea uwezo watendaji wake pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles