25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

TPA kurasimisha bandari bubu Kigoma

ESTHER MBUSSI-KIGOMA

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) Kanda ya Ziwa Tanganyika, iko kwenye mchakato wa kurasimisha bandari ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkuu wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, alisema lengo la hatua hiyo ni kuzifanya bandari hizo zifanye kazi kulingana na kanuni na taratibu za kisheria hivyo kuimarisha ulinzi na usalama.

“Utaratibu wa urasimishaji na kuzifunga bandari hizo bubu unaendelea na ukishamalizika tutazitangaza,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, Msese alisema katika Bandari ya Kigoma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji lakini wamejipanga kukabiliana nazo kwa kuzitatua kimkakati.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kupungua kwa shehena iendayo nchi jirani za Congo na Burundi ambapo mkakati wa kutatua changamoto hiyo no kuendelea na juhudi za kutafuta masoko mapya na kuvutia yaliyopo.

“Changamoto nyingine ni ufanisi mdogo wa Shirika la Reli nchini (TRC), lakini mazungumzo ya pamoja kati ya Bandari ya Kigoma na TRC ili kuweza kuboresha miundombinu ya Reli kwa nia ya kuboresha huduma za usafirishaji,” alisema Msese.

Akizungumzia huduma zinazotolewa na Bandari ya Kigoma, Msese alisema inatoa huduma kwa wateja aina mbili yaani wenye meli na wenye mizigo na nchi zinazohudumiwa na bandari hiyo ni Congo na Burundi.

Alisema bandari hiyo pia inahudumia shehena mchanganyiko, mafuta na makasha ambapo shehena hiyo imekuwa ikiongezeka licha ya matatizo ya njia ya usafirishaji hususani reli.


“Lakini pia katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi, mamlaka imeendelea kuboresha Bandari ya Kigoma kwa kufanya maboresho ya gati la abiria na upembuzi yakinifu ulishafanywa Kampuni ya M/S Royal Haskoning ya Uholanzi katika gati la mizigo umeshakamilika.

“Shirika la Misaada la Japan (JICA), litatekeleza mradi wa uboreshaji wa gati la abiria na ghala la kuhifadhia mizigo ambapo ujenzi huo utaanza Julai mwaka huu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles