Na Mwandishi Wetu, Mtwara
Mamlaka ya Dawa ,Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Kanda ya Kusini imemkamata, Jamaly Sadick baada ya kuwekewa mtego akiuza dawa za serikali za uzazi wa mpango
Taatifa iliyotolewa leo Febriari Mosi na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza, imesema kuwa Januari 31, mwaka huu waliweka mtego, Wilaya ya Newala Mji na kumnasa, Sadick akiuza dawa hizo.
“Baada ya kuwekeza katika taarifa za kiintelijensia tulifanikiwa kumkamata akiuza dawa hizo. Dawa hizo ni Medroxy Progesterone (vichupa 60) na Microgynon pills (vidonge 3360) zote zikiwa na thamani yaSh.300,000.
“Mtuhumiwa na mtoto wake wamefunguliwa jalada polisi RB No.NL/RB/94/221 na yuko ndani kwa hatua zaidi kisheria,” imeeleza taarifa hiyo.