22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

TIGO YAWAZAWADIA SIMU WASHINDI JAZA UJAZWE

 

 

Na MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania, imekabidhi zawadi za simu za smartphone aina ya Tecno S 1 kwa washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, iliyozinduliwa Agosti mosi, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makabidhiano ya washindi 38 kwa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Meneja Mgunduzi wa Tigo, Jackline Nnunduma, alisema wanatoa zawadi ya simu kwa mshindi kila saa moja katika saa 24 kwa siku.

“Kila mteja wa Tigo anaweza kujishindia simu hii aina ya Tecno S 1 kila anapoongeza muda wa maongezi ambapo ataingia katika droo, leo hii tunakabidhi simu kwa washindi 38 wa hapa Dar es Salaam, tayari tuna washindi 120 kwa Tanzania nzima kutoka mikoa ya Dodoma, Tanga, Kagera, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Singida na Zanzibar,” alisema.

Alisema Tigo inawajali wateja wake kwa kuwa wanawaunga mkono katika kutumia bidhaa na huduma zao na kuwaomba waendelee kutumia huduma hizo na kila mmoja ana fursa ya kujishindia simu hizo.

Mmoja wa washindi hao, Jachinda Kalinga, aliishukuru Tigo kwa kumzawadia simu hiyo ya Tecno S 1 huku akiwataka wale ambao hawatumii mtandao huo kuanza kutumia ili wapate fursa ya kujishindia zawadi ya simu.

 

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles