23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DONDOO

Man United

UONGOZI wa klabu ya Manchester United umeweka wazi kuwa hauna mpango wa kuongeza dau zaidi ya pauni milioni 90 ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale. Nyota huyo alijiunga na Man United kwa pauni milioni 86, akitokea Tottenham.

Real Madrid

KWA mujibu wa gazeti la AS nchini Hispania, limeweka wazi kuwa kiungo wa klabu ya Real Madrid, Isco, amemalizana na klabu hiyo kwa kuongeza mkataba wa miaka mitano. Nyota huyo alikuwa anahusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Man United.

Tottenham

KLABU ya Tottenham ipo kwenye hatua za mwisho kumalizana na nyota wa klabu ya Ajax ambaye anacheza nafasi ya ulinzi, Davinson Sanchez. Hata hivyo, wapo kwenye ushindani dhidi ya wapinzani wao, Inter Milan, ambao wameonesha nia ya kuitaka saini ya mchezaji huyo.

Barcelona

KLABU ya Barcelona hadi sasa inahangaika kumtafuta mchezaji ambaye ataziba nafasi ya Neymar, aliyejiunga na PSG, hivyo wapo kwenye mipango ya kuwania saini ya nyota wa klabu ya Tottenham, Christian Eriksen, lakini Tottenham wamedai mchezaji huyo hauzwi.

AS Roma

KLABU ya AS Roma imesema ipo tayari kumsajili nyota wa klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez, lakini ofa yao haiwezi kuzidi pauni milioni 32. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Arsenal, lakini Wenger amedai hakuna mazungumzo dhidi ya mchezaji huyo.

Barcelona

NYOTA wa klabu ya Borussia Dortmund, Ousmane Dembele, anaweza kuonekana akiwa amevaa uzi wa klabu ya Barcelona katika kipindi hiki cha msimu mpya, kutokana na klabu hiyo kufikia makubaliano ya awali na mchezaji huyo juu ya uhamisho wake.

Atletico Madrid

WAKALA wa Javier Pastore, Marcelo Simonian, amewasili kwenye viwanja vya Atletico Madrid ili kufanya mazungumzo na klabu hiyo juu ya uhamisho wa mteja wake. Hata hivyo, PSG wamesema wanaweza kumuacha mchezaji huyo akijiunga na Atletico Madrid kwa kubadilishana na kipa wa timu hiyo, Jan Oblak.

Juventus

UONGOZI wa klabu ya Juventus umejitosa kuwania saini ya kiungo wa klabu ya AS Roma, Kevin Strootman. Juventus wamedai wanataka kumsajili mchezaji huyo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. AS Roma wamesema watamuacha mchezaji huyo kwa Euro milioni 45.

Southampton

KLABU ya Southampton imeweka wazi nia ya kutaka kumsajili nyota wa klabu ya Celtic, Stuart Armstrong, klabu hiyo imedai kuwa ipo tayari kuweka mezani kitita cha pauni milioni 3 ili kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo katika kipindi hiki cha usajili.

Arsenal

HATIMAYE klabu ya Arsenal imetangaza kutaka kuvunja benki yao ili kuweza kumbakisha mshambuliaji wao, Alexis Sanchez. Arsenal wamesema wapo tayari kumlipa pauni 300,000 kwa wiki. Nyota huyo amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na klabu ya PSG na Man City.

Barcelona

KLABU ya Barcelona imejitosa kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Marco Asensio, huku wakijiandaa kuweka mezani pauni milioni 72 ili kumsajili mchezaji huyo. Barcelona inahangaika kutafuta mchezaji ambaye ataziba nafasi ya Neymar.

Juventus

JUVENTUS wamejiingiza kwenye vita ya kuwania saini ya nyota wa klabu ya Barcelona, Sergi Roberto, klabu nyingine ambazo zinawania saini ya mchezaji huyo ni pamoja na Manchester United na Chelsea. Mchezaji huyo alitangaza kuwa anataka kuondoka kipindi hiki cha kiangazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles