22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

MAUMIVU The Pain

 

 

ILIPOISHIA…

“Naitwa Christina ni mmoja wa vijana wa Patii…hatuwezi kuongea mengi kwa sasa lakini fahamu kwamba mimi ndiye niliyekuokoa, sijapendezwa na mateso uliyokuwa ukiyapata mwanamume mzuri kama wewe hivyo niliamua kukusaidia.

“Bado ninahitaji kukusaidia zaidi, lakini lazima uwe msiri sana, nimeamua kuisaliti kazi yangu kwa huruma yangu kwako, nitakachokifanya ni kukufanyia mipango ya safari ya kurudi nyumbani kwenu mapema, ukipata nafuu tu, utaondoka.

“Kila kitu niachie mimi, ukiwa Tanzania tutawasiliana na kupanga jinsi ya kumuokoa Joe, najua mahali alipo, maagizo yote nitamwachia huyo nesi anayekuhudumia, anaitwa Julieth,” Christina alisema maneno hayo haraka-haraka.

Pius hakuamini!

SASA ENDELEA…

SIKU nzima Joe alishinda chumbani akiwa na Queen lakini hakuonyesha kuwa na furaha kabisa, mapenzi yake na Queen yalishamiri zaidi. Hawakuwa kama wapenzi wa kulazimishwa kama ilivyokuwa awali, sasa walikuwa wanapendana kiukweli ingawa Joe alishindwa kuamua kuuweka wapi moyo wake kutokana na kumpenda zaidi Ester wake.

Siku hiyo alikuwa tofauti sana, hakumshumbua Queen, Joe alikuwa kimya karibu muda wote.

“Una nini Joe?”

“Naona sasa mapenzi yetu yamekwisha Queen, uliniambia utaniambia kila kitu kuhusu mahali hapa, ukaniahidi utanisaidia niondoke, lakini mpaka sasa hakuna unachokifanya zaidi ya mapenzi tu, kwani nimekuambia nahitaji kustarehe bila kujua mustakabali wa maisha yangu?

“Queen nimekubali kuishi na wewe na ni lazima tutoroke, mbinu zote unazo wewe, lakini hutaki kunishirikisha au umenichoma nini, maana nasikia mkuu anahitaji kuonana na mimi,” Joe akasema.

“Usijali mpenzi wangu, onana naye kwanza, halafu ukirudi utaniambia aliyokuambia na hapo ndipo nitapokupa kila kitu na mipango ya kutoroka itaanza mara moja!” Queen akasema.

Kabla hajamalizia sentesi yake, ghafla mlango ulifunguliwa, akaingia kijana mmoja mwenye mwili wa mazoezi, aliyevaa suruali ya jeans nyeusi na fulana ya kukata mikono nyeusi, miwani mweusi, akiwa na bastola nyeusi.

Weusi ulitawala mwilini mwake.

“Joe hutakiwi kujigusa na unatakiwa kufuata kila nitakachokueleza!” kijana huyo akasema.

Joe akatoa macho kwa mshangao, ishara iliyokuwa mbele yake ni kwamba alikuwa akikiendea kifo chake. Hilo alilifikiria, lakini pia aliwaza jinsi ya kupambana. Alikuwa tayari kupambana.

Joe akatoa macho kwa mshangao, ishara iliyokuwa mbele yake ni kwamba alikuwa akikiendea kifo chake. Hilo alilifikiria, lakini pia aliwaza jinsi ya kupambana. Alikuwa tayari kupambana.

Akayarudisha macho yake kwa Queen, naye alikuwa akistaajabu kilichotokea.

“We’ ni nani?” Queen akauliza.

“Huwezi kunijua!”

“Sasa kwanini unatutenda hivi?”

“Siyo mimi ni amri ya mkuu!”

“Nani?”

“Tuna wakuu wangapi hapa?”

“Mmoja na kila mtu anafahamu wazi kwamba tuna mkuu mmoja ila nataka kuhakikisha kama ni kweli aliyekutuma ni yeye!”

“Unataka kujua, sasa nakwambia kwamba nimetumwa na Patii na kwa jinsi ulivyonichelewesha kufanya kazi yake nakuahidi utajutia!”

Queen akakaa kimya!

Azungumze nini tena?

Joe akanyanyua mikono yake chini, kisha akatangulia mbele akielekezwa njia na yule kijana ambapo alimtembeza katika korido kadhaa kabla ya kupanda lifti na kwenda ghorofa ya juu zaidi.

Hakuzungumza naye kitu chochote, walipofika mlango ukafunguka, wakatoka na kukatiza kwenye korido nyingine kisha wakaingia kwenye chumba kimoja, chenye mlango wa kioo cheusi.

Mlango haukufunguliwa, ulifunguka wenyewe baada ya wao kuukaribia. Kilikuwa chumba kikubwa, chenye kila kitu cheusi, kuanzia zulia lililokuwa chini hadi glasi za kunywea maji!

Weusi ulitawala katika chumba kile.

Joe akabaki akishangaa, lakini kichwani mwake aliendelea kuwaza jinsi ambavyo angeweza kutoroka. Ilikuwa kazi kubwa sana, hasa ukizingatia alikuwa peke yake na taarifa alizokuwa amepata ni kwamba hata Pius naye alikuwa mikononi mwa Patii.

“Kuna uwezekano mkubwa sana leo nikafa, lakini kama nilivyoapa mwanzoni, siwezi kufa kikondoo kabisa! Siwezi…mimi ni mwanaume na ni lazima nionyeshe uanaume wangu, haiwezekani kabisa nikafa huku najiona, najua nitakufa lakini lazima nife na mtu…najiamini sana, najijua…Inspekta Joe…” Joe aliwaza huku akijitahidi sana kukwepa sura ya mkewe iliyokuwa ikimtokea kila wakati alipokuwa katikati ya mawazo hayo.

“Sikukusikia mke wangu, pengine majaribu haya nisingekutana nayo, naona kabisa kifo changu sasa, nakufa mbele yangu kukiwa na sura yako, nakupenda sana Ester wangu, sitaacha kukupenda siku zote za maisha yangu maana ni kweli nakupenda sana mama…wewe ni taa ya maisha yangu, nitaendelea kukupenda wewe na mwanangu siku zote…nawapenda na nitawapenda daima…” akili ya Joe ilishabadilika sasa, alikuwa akiwaza juu ya kifo chake baaasi!

“Kaa hapo!” akasikia sauti ikimuamrisha aketi.

Akaketi.

“Hutakiwi kujigusa na yakupasa ufuate maelekezo yote utakayoyasikia…nakutakia utekelezeaji mwema!” yule kijana alipomaliza kusema maneno hayo akaondoka na kumwacha Joe akiwa peke yake katika kile chumba, mawazo tele yakamjaa kichwani.

Kwamba angechomwa akiwa ndani ya chumba kile!

Au angelishwa sumu!

Angepigwa!

Aliwaza kuhusu kifo!

Alijua ni siku yake ya kufa! Ghafla akiwa katika ya mawazo akashangaa kusikia kama muungurumo mkali na mtikisiko ambao hakujua ulikuwa ukitokea wapi kisha akasikia sauti ya taratibu sana.

“Habari yako Joe!” sauti hiyo ilikuwa ikitokea katika spika kubwa zilizokuwa zimezunguka chumba hicho.

Joe hakuitika!

Hakukuwa na mtu!

“Nakusalimia Joe…” sasa aliweza kuikumbuka sauti hii vizuri.

Ilikuwa ni sauti ya Patii ambaye hata hivyo hakuonekana sehemu yoyote ndani ya chumba kile, ni wazi kwamba alikuwa amejificha mahali na alikuwa akitumia kipaza sauti kuzungumza naye.

Je, nini kitatokea? Usikose kufuatilia Jumamosi ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles