THE ROCK, VIN DIESEL KUMALIZA TOFAUTI ZAO

0
892

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa filamu, Dwayne Johnson maarufu kwa jina la The Rock, ameweka wazi kuwa yupo kwenye mipango ya kumaliza tofauti zake na Vin Diesel.

Inasemekana kuwa wakali hao wa filamu waliingia kwenye mgogoro tangu Agosti 2016, hadi sasa hawapo katika mazungumzo mazuri, hivyo The Rock amedai anatarajia kukaa nchini na Vin Diesel kwa ajili ya kumaliza tofauti zao.

“Mimi na Vin Diesel tunatarajia kukutana na kufanya mazungumzo ili kuona uwezekano wa kumaliza mgogoro wetu, kwa sasa naweza kusema sina tatizo na msanii huyo lakini lazima tukutane na kuyamaliza.

“Najua kuna vitu vya msingi ambavyo tulikuwa tunapishana na kila mmoja alikuwa na misimamo yake, kwa sasa nipo tayari kufanya kazi na msanii huyo endapo atakuwa tayari,” alisema The Rock.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here