29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

BIEBER ATUMIA SAA 100 KUCHORA ‘TATTOO’

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuonesha michoro yake mipya mwilini na kudai kwamba alitumia saa 100 kukamilisha kuichora.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 24, mwenye asili ya nchini Canada, aliiweka picha hiyo juzi na kuandika “Zaidi ya saa 100 za kuchora michoro mwilini mwangu hadi kuweza kukamilika na kuwa kama hivi nilivyo sasa.

“Nadhani michoro hii hakuna inayomhusu ila ni mimi mwenyewe, siku zote nimekuwa nikipenda michoro mwilini, hivyo ni maamuzi yangu kufanya nikipendacho,” alisema Bieber.

Hata hivyo, msanii huyo amesema kwa sasa anaweza kutembea kifua wazi kwa ajili ya kuonesha michoro hiyo. Awali alikuwa na michoro michache tofauti na ilivyo sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles