Thailand: Mfalme Vajiralongkorn amuoa mlinzi wake na kumtawaza kuwa Malkia

0
708

Mfalme wa Thailand Maha Vajiralongkorn amemuoa Naibu Mkuu wa kikosi cha walinzi wake  na kumpa cheo cha malkia, imesema taarifa ya ufalme huo.

Tangazo hilo la kushitukiza limetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza Jumamosi, wakati atakapochukua wadhfa wake.

Mfalme Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa sana kilichotokea mwaka 2016.

Amekwisha wataliki wanawake mara tatu na ana watoto saba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here