23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA yazitaka Taasisi kudhibiti taka hatarishi

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

SERIKALI imewataka wadau wa sekta ya mawasiliano nchini kuzitunza nakuzitekeza taka hatarishi zinazotokana na vifaa vya kieletroniki.

Wito huo umetolewa leo Machi 20, 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kongamano la wadau wa sekta ya Mawasiliano amesema takwimu za taka hatarishi zinazotokana na mabaki ya vifaa vya masiliano zimekuwa zikiongezeka hali inayo pelekea hatari za kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

“Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya taka milioni 7.7 za kieletroniki huzalishwa kila mwaka,” amesema Nape.

Waziri Nape amesema lengo la kongamano hilo linazojumuisha nchi 17 za Afrika nikuona ni jinsi gani ya kupunguza taka hizo kwa kutunga sheria na miongozo ya punguza taka hizo.

Ameongezea kuwa lengo nikuona matakwa ya kisheria yanafuatwa katika kuteketeza taka hizo.

“Nchi za Afrika Mashariki zimekuja Tanzania ikiwa ni mwenyeji kujadili namna yakutokomeza na kuharibu taka za kieletroniki,” amesema Nape.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawassiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabir Bakari amezitaka taasisi mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu kuzifanyia tafiti taka hizo hatarishi ilikuweza kuondokana na tatizo lauharibifu wa mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles