24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TBL Group yawageukia wajasiariamali wadogo

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Group, Gareth Jones
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Group, Gareth Jones

Na PAULINA KEBAKI,DAR ES SALAAM

WAFANYABIASHARA wadogo wanaouza bidhaa za viwanda vya Kampuni ya TBL Group  nchi nzima wanatarajia kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali yaliyoondaliwa na kampuni hiyo kupitia mpango wa kuendeleza wajasiriamali wadogo inaoshirikiana nao ujulikanao kama ‘Retail Development Programme (RDP).

Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Group, Gareth Jones, alisema Dar es Salaam jana kuwa mafunzo hayo katika awamu ya kwanza yatawafikia zaidi ya wafanyabiashara  1,838 kutoka  kanda mbalimbali za mauzo ya kampuni hiyo nchi nzima.

“Mafunzo hayo yataendelea kwa  miezi mitatu kuanzia sasa  ikiwa  ni mwendelezo wa mkakati wa kampuni wa kuwawezesha wabia  inaoshirikiana nao biashara kwa kufikisha bidhaa inazozalisha kwa walaji wa mwisho.

“Lengo ni kuwawezesha   waendeshe biashara zao kwa weledi na kupata mafanikio katika biashara zao” alisema Jones na kuongeza:

“Mtazamo na moja ya  malengo ya kampuni mama ya SABMiller ni kujenga ‘Dunia Yenye Nuru Njema’.

“Hii imelenga kuharakisha ukuaji wa maendeleo ya  jamii kwa kuhakikisha wabia  wanaouza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyake hususan wafanyabiashara wadogo wanawezeshwa kustawisha biashara zao  ikiwamo kuwawezesha kuishi maisha bora na familia kupitia biashara  zao na kutoa mchango wa kuendeleza jamii wanazoishi na kufanyia biashara zao”.

Mafunzo  yatakayotolewa kwa wafanyabiashara hao  ni kuhusiana na mbinu za kufanikisha mauzo na nidhamu katika matumizi ya fedha, mahesabu sahihi katika biashara.

Mengine ni  utunzaji sahihi wa vitabu vya hesabu na mbinu za kukabiliana na ushindani wa biashara ya uuzaji vinywaji  na ujasiriamali kwa ujumla.

Katika mafunzo hayo, wafanyabiashara  wanafundishwa masuala ya usafi na mazingira katika maeneo yao ya biashara  na kanuni nyinginezo ikiwamo taratibu za uendeshaji biashara  kwa kushirikiana  na kampuni ya TBL Group na kutambua bidhaa zinazozalishwa na kampuni  hiyo na kampuni zake tanzu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles