24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Tausi Likokola azindua vazi la amani

TAUS LIKOKOLANA CHRISTOPHER MSEKENA

ONYESHO la mavazi ‘Fashion for Peace’ limezindua vazi maalumu kwa ajili ya kuhamasisha amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.

Onyesho hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa King Solomon, Dar es Salaam liliwajumuisha wabunifu, Mustafa Hassanali, Martin Kadinda na Kiki Zimba.

Onyesho hilo lilifunguliwa na mwanamitindo wa Tanzania anayefanya kazi zake barani Ulaya, Tausi Likokola, aliyevalia vazi la mbunifu Kiki Zimba kwa kuzingatia umuhimu wa amani.

Martin Kadinda alibuni nguo zilizovaliwa na wanamitindo wa kiume, nguo hizo nyingi zikiwa na rangi ya njano na nakshi za kijani zililenga kubeba rangi tatu kuu zilizopo katika bendera ya taifa.

Naye Mustafa Hassanali, nguo zake zilipambwa na rangi ya njano na dhahabu pamoja na vito vilivyotengenezwa na ‘Phoebe Jewellery’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles