MSANII wa Bongo Fleva nchini, Abdu Kiba, amedai kufanya kazi ya muziki na ndugu wa damu moja, kumemsaidia kutambulika haraka kwenye soko la muziki ndani na nje ya nchi.
Abdu Kiba anayeendelea kutamba na wimbo mpya wa ‘Ayaya’ aliomshirikisha Hellen Magashi ‘Rubby’, amesema ni fahari kwake kwa kuwa kazi yake ya muziki imepokelewa kwa urahisi.
“Kuna faida kubwa sana ya kufanya kazi na ndugu hasa anapokuwa na mashabiki wengi kama ilivyo kwa kaka yangu, Ally Kiba.
“Umaarufu wa Ally Kiba umenisaidia sana kimuziki, mashabiki wengi waliposikia mdogo wake anaimba walipata hamu ya kujua uwezo wangu na sasa nina idadi kubwa ya mashabiki tofauti na nilivyodhani kwamba ingekuwa ngumu kwangu,” alisema Abdu Kiba.