24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Tasac yasisitiza uzingatiaji wa Sheria majini

Na Anna Ruhasha, Geita

Wamiliki, watumiaji na wasimamizi wa vyombo vya majini wamekumbushwa kufuata sheria zilizowekwa wakati wa utumiaji wa vyombo hivyo hasa kutumia makoti yanayo akisi mwanga ili panapotokea ajari za majini iwe rahisi katika uokoaji.

Wito huo  umetolewa na ofisa wa Shirika la Uwakala wa meli Tanzania mkoa wa Geita (TASAC )Rashid Katonga wakati akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya Nne ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Aidha amesema  shilika hilo lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge ya mwaka 2017, lilianzishwa kutoka na mgawanyiko wa SUMATRA, kutokana na sheria hiyo amesema  ilipelekea TASAC kuanza kutoa huduma za utendaji katika kutekeleza shughuli za utendaji, ulinzi na usalama wa usafirishaji majini.

Pia Katonga ametaja shughuli zinazosimamiwa na TASAC kuwa ni huduma za madini,  Vipuli, Mitambo, Vilainishi, Mafuta, Nafaka pamoja na Gesi.

“TASAC inafanya kazi katika mikoa inayopakana na ziwa au bahari ambapo tupo mkoani Geita, Mwanza, Musoma, Kigoma, Katavi, Dar es Salaam, Pwani, Rukwa,  Lindi na baadhi ya mipaka hapa nchini ikiwamo Holili,”amesema.

Amesema, mkoa wa Geita unatumia vyombo vingi vidogo vya majini ikiwamo mitumbwi na boti vinavyosafirisha abiria na siyo meli ambapo amewataka watumiaji kuzingatia sheria ya matumizi kwa abiria kutumia jaketi linaloasiki mwanga wakati wa safari  nakusisitiza lazima ziwezimekidhi viwango, kwa kuhakisi mwanga, pia ziwe na  filimbi na mikanda ili iwe raisi katika ukoaji pindi panatokea ajari ya majini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles