28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Tarura wamkera mkuu wa mkoa

Na FLORENCE SANAWA-MTWARA

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, amechukizwa na utendaji wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura), baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Hali hiyo imekuja baada ya mkuu huyo wa mkoa kufanya ziara ya kutembelea barabara hizo na kubaini kuwapo kwa vifusi vilivyokaa muda mrefu barabarani na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara.

Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mtwara, Byakanwa alisema haridhishwi na utendaji wa wakala huyo kwa kuwa wameshindwa kutimiza majukumu yao.

Kutokana na hali hiyo, mkuu huyo wa mkoa aliahidi kuunda kamati ya uchunguzi ili kujua jinsi Tarura wanavyofanya kazi.

“Kwa hiyo, kamati hiyo itafanya kazi ndani ya wiki mbili na kukabidhi ripoti kwangu ili kujua wakandarasi wanapatikanaje na wanalipwa kiasi gani ili kuweza kuchukua hatua.

“Yaani, kitendo cha barabara za halmashuri kuwa mbovu na kushindwa kupitika kwa sababu ya Tarura inapelekea wananchi wailaumu Serikali bila sababu za msingi.

“Yote mmejieleza sasa subirini kamati iwahoji ndiyo itakuja na jibu kwa sababu hatuwezi kuwaacha kama wanyama wasiotawalika.

“Hatuwezi kulifumbia macho suala hilo kwa sababu sote tunajua umuhimu wa barabara, hatuwezi kukaa kimya wakati njia hazipitiki wakati wa mvua wala kiangazi,” alisema Byakanwa.


Naye Mratibu wa Tarura, Mkoa wa Mtwara, Silaji Mbuta, alisema wamekuwa wakipangiwa bajeti ndogo ya asilimia 30 na hivyo kushindwa kutekeleza baadhi ya miradi yao.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, alisema makandarasi wa Tarura wamekuwa wakishindwa kutekeleza baadhi ya miradi ya barabara bila sababu za msingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles