25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Kamuzora azungumzia chaneli ya utalii 

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya Tanzania Safari Channel, Profesa Faustin Kamuzora, amesema kwamba wadau wa utalii nchini wamekubaliana kutoa bajeti ya Sh bilioni tano ili kufanikisha uendeshaji wa runinga hiyo ya Serikali mahususi kwa kutangaza utalii na vivutio vyake hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Prof Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), alisema fedha hizo zitatumika ndani ya miezi sita katika kununua vifaa, kuweka wataalamu na kununua vipindi.

Prof. Kamuzora ameongeza kwamba ripoti ya kamati hiyo juu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali itakabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 2, mwakani.

“Kwa sasa mpaka mienzi sita ijayo ili kuweza kufanikisha mipango ya uendeshaji wa kituo hicho cha runinga tunahitaji kama Sh bilioni tano, ambapo kwenye kikao chetu wadau wamekubali kutoa kiasi hicho, TBC tayari ilikuwa na bajeti yake na mchango wao pia ni zaidi ya bajeti kwa kuwa wao wanaendesha runinga hiyo,” alisema.

Aliongeza kwamba rasilimali hizo za wadau hao zitatumika kununulia vifaa na wataalamu wa kutosha na kupata vipindi vya kununua na kutengeneza vipya kwa kutumia wataalamu watakaoajiriwa na vifaa vitakavyonunuliwa.

Mwenyekiti huyo aliweka wazi kwamba kwa sasa runinga hiyo haina maudhui ya kutosha, lakini wadau wamejipanga ili kuhakikisha kwamba ndani ya mienzi sita suala hilo linapatiwa ufumbuzi ambapo kutakuwa na maudhui ya kutosha.

“Wadau wakubwa wote wameonyesha utayari na wamekubali kwamba kwenye mienzi sita iliyobakia ya bajeti hii ya sasa watatenga fedha ya kutosha na kwenye bajeti inayofuata ya 2019/2020 watatenga fedha kwa ajili hiyo,” alieleza.

Aliwataja baadhi ya wajumbe wa kamati kwamba ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tanapa, Tawa, Ngorongoro, TTB, TCRA, TBC, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Msemaji wa Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles