21.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

TANZANIA YARIDHIA MPANGO WA KUBORESHA MISITU

Patricia Kimelemeta, Dar es SalaamTanzania ni miongoni mwa nchi 23 za Afrika zilizoridhia mpango wa Umoja wa Mataifa (UN) wa kuhifadhi, kulinda na kuboresha misitu.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa uzinduzi wa tamko la pamoja la kushirikiana na wadau mbalimbali Afrika na duniani kwa ujumla katika kuhifadhi na kuendeleza misitu (Afrika100).

Tamko hilo limetolewa katika Msitu wa Kazimzumbwi wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani ambapo pamoja na mambo mengine, Hasunga amesema nchi za Afrika ziliahidi kuhifadhi hekta milioni 100 kuanzia mwaka huu hadi ifikapo mwaka 2030.

“Kila mwaka mazao ya misutu yanachangia pato la taifa kwa asilimia 3.9, hivyo basi tunapaswa kuboresha mazingira ya misitu ikiwa ni pamoja na kulinda, kuweka miundombinu bora ya barabara ili kuvutia watalii, hali ambayo itatuongezea mapato,” amesema Hasunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles