30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 16, 2021

CCM YASHINDA KATA MBILI LINDI

 

Hadija Omary, LindiChama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi kimeshinda kwa kushinda katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Madiwani katika kata za Nachingwea na Namichiga.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa CCM Kata ya Namichiga, Mikidadi Mtauna alishinda kwa kura 781 huku mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salama Wambamba akiambulia kura 209.

Kwa mujibu wa Ofisa Uchaguzi Wilaya ya Ruangwa, Yusuph Chilumba waliojiandikisha kupiga kura katika Kata ya Namichiga walikuwa 2,874, kura zilizopigwa 1,020, kura halali 990 kura zilizoharibika 30.

Katika Kata ya Nachingwea, Bakari Mpanyangura alishinda kwa kura 1,116, Mwanahamisi Mshamu wa Chadema alipata kura 308, huku mgombea wa Chama cha Wananchi (Cuf) Abuu Bakari Kondo akipata kura 18.

Akizungumzia uchaguzi huo, Chilumba amesema Nachingwea idadi ya waliojiandikisha walikuwa 6,466 kura zilizopigwa 1,466, na kura halali 1,442 huku kura zilizoharibika zikiwa 24.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,870FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles