23.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kupokea wageni 1,200 Mkutano wa Raslimali Watu

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Tanzania inatarajia kupokea wageni zaidi 1200 kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika kwenye mkutano wa Wakuu wa nchi kujadili mtaji wa Rasilimali Watu utakaofanyika Julai 25 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizumgumza na Waandishi wa Habari leo Julai 21, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkutano utafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa Mwalimu Julias Nyerere (JNICC) na kwamba ni muhimuni kwasababu ni sehemu ya kutangaza utalii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo.

Amesema mkutano huo wenye lengo la kujadili mtaji wa rasilimali watu na ukuaji uchumi imara kwa Bara la Afrika.

“Kupitia mkutano huu mkubwa wenye wageni zaidi ya 1,200 wa mtaji rasilimali watu Bara la Afrika ni maslahi ya uchumi wa nchi na kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini na ni fursa kwa nchi yetu,” amesema Chalamila.

Amesema hoteli zaidi ya 40 zinatarajia kupokea wageni na kwamba walikutana na wamiliki wanaohusika na hoteli hizo kuboresha mazingira na wameboresha kwa sababu utalii ni ajenda muhimu katika mkutano huo.

“Wageni hawa wanatembelea sehemu mbalimbali ni lazima tuboreshe mazingira ikiwa hoteli, sehemu za fukwe na kuandaa vyakula vya asili ya Tanzania,” amesema Chalamila.

Aidha, amesema zaidi ya wajasiriamali 100 watashiriki kwenye mkutano huo kwa kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa ikiwamo utamaduni pia wafanyabiashara kutoka nchi hizo watashiriki.

Amesema mkutano huo ni somo kubwa kwa nchi za Afrika na kujenga upya Afrika na kwamba baada ya mkutano huo wataondoka na azimio la Dar es Salaam.

Amewaomba wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa kipindi hicho cha mkutano wa wakuu wa nchi wadumishe utulivu, amani, ukharimu na kujitahidi kufanya usafi wa mazingira.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano JNICC, Ephraim Mafuru amesema maandalizi kuelekea mkutano huo yamekamilika ambapo vifaa vyote vimekamilika ikiwa ni sambamba na ulizi na usalama.

Mkutano huu umeandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles