28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tanroad yatumia Tril. 1.37 kukamilisha ujenzi wa barabara 14

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), Rogatus Mativila amesema wamekamilisha miradi ya ujenzi wa barabara 14 zenye urefu wa kilometa 883 kwa gharama Sh trilioni 1.37.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), Mhandisi Rogatus Mativila akizungumza na Waandishi wa Habari

Kauli hiyo ameitoa Jumamosi Oktoba 29,2022 wakati wa akielezea utekelezaji wa majukumu ya Tanroad na vipaumbele kwa mwaka 2022/2023.

“Miradi hiyo imekamilika katika kipindi cha Aprili 2021 hadi sasa yaani ndani kipindi cha Awamu ya Sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Mhandisi Matibila.

Aidha, Mativila amesema jumla ya miradi mitatu ya madaraja makubwa ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji kwa kwa gharama ya Sh bilioni 701.

Mhandisi Mativila amesema miradi 44 ya barabara yenye urefu wa Kilometa 1,523 na gharama ya Sh Trilioni 3.8 ipo katika hatua mbali mbali ya ujenzi nchi nzima.

Kuhusu usanifu wa barabara amesema unaangaliwa idadi ya magari yatakayotumiwa na barabara husika.

Ametoa mfano wakati barabara ya Iringa kwenda Dodoma inajengwa, mwaka 2011/2012 ilikuwa haipo ya lami na ilihitajika kujengwa katika kiwango cha lami kwa wakati huo.

“Katika ujenzi wa barabara tuna classes za traffic (madaraja), traffic loading, ile (Iringa hadi Dodoma), iliwekwa class (daraja) ambalo lilikuwa ni chini kwasababu ya fedha zilizokuwa zipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles