31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Bado Watanzania hawali nyama vya kutosha-TMB

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Bodi ya Nyama Tanzania(TMB) imesema takwimu zinaonyesha bado Mtanzania mmoja anakula kilo 15 za nyama kwa mwaka badala ya kilo 50 zinazoshauriwa kitaalam.

Pia imesema jumla ya tani 10,415 za nyama ziliuzwa nje ya nchi katika mwaka 2020/2021 ambazo ziliipatia Tanzania Sh bilioni 96.

Mkurugenzi wa Bodi ya Nyama(TMB), Dk. Daniel Mushi akizungumza na Waandishi wa Habari.

Hayo yameelezwa Oktoba 28,2022 na Msajili wa Bodi hiyo, Dk. Daniel Mushi wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Msajili huyo amesema kuwa takwimu zinaonyesha bado mtanzania mmoja anakula kilo 15 za nyama kwa mwaka badala ya kilo 50 zinazoshauriwa kitaalam.

“Watanzania wengi tunahitaji kuboresha afya zetu kwa kula nyama, kiasi ambacho kinachoruhusiwa na kupendekezwa,” amesema Dk. Mushi.

Dk. Mushi amesema mkakati wao kwa mwaka 2022/2023 ni kuongeza kiasi cha nyama kinachouzwa nje ya nchi ambapo hadi sasa wanauza kwa kiasi kikubwa katika nchi za Mashariki ya Kati.

Amesema kwa mwaka wa fedha uliopita waliuza nyama nje ya nchi tani 10,415.

“Ni kiasi ambacho hatujawahi kufikia,kiasi kikubwa cha fedha kimepatikana kutokana na kuuza nyama nje ya nchi,”amesema.

“Lengo la bodi hiyo ni kuhakikisha kuwa wanaongeza uuzaji wa nyama nje ya nchi hadi kufikia tani 16,000 kila mwaka ifikapo mwaka 2026,”amesema Dk. Mushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles