29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

TANESCO YAWAKATIA UMEME POLISI MOSHI

                                                      |Upendo Mosha, MoshiShirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Kilimanjaro, limekata umeme katika Ofisi ya Jeshi la Polisi katika Mji Mdogo wa Himo wilayani Moshi, kutokana na madai ya malimbikizo ya zaidi ya Sh bilioni tatu.

Hatua hiyo imetokana na operesheni ya kusitisha kutoa huduma ya umeme katika taasisi mbalimbali za serikali.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, amesema operesheni hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu wanaoongoza wakiwamo polisi, Jeshi la Magereza, hospitali za serikali, Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Wilaya za Same na Mwanga.

“Shirika litaanza kusitisha huduma ya umeme katika taasisi hizo mara moja kutokana na kushindwa kulipa madeni yao kwa wakati na kuisababishia mamlaka hiyo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi na kuboresha huduma zake kwa wananchi,” amesema.

Aidha, amesema shirika hilo limetoa ofa maalumu ya punguzo kwa kipindi hiki endapo mteja anayedaiwa atalipia deni lake na kwamba atasamehewa gharama za riba zinazoongezeka kutokana na kulimbikiza madeni kwa muda mrefu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,474FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles