28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO yatakiwa kurekebisha transfoma nchi nzima

Na Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amelitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO ) kuhakikisha wanarekebisha miundombinu hasa transfoma nchi nzima.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu huyo Januari 26,2024 alipotembelea transfoma mbalimbali zenye changamoto katika Wilaya ya Temeke.

Amesema serikali imefanya uwekezaji mkubwa ili kuhakikisha wananchi wanapata umeme hivyo hawatavumilia yeyote atakaesabaisha uharibufu kwenye miundombinu hiyo.

“Nawaelekeza TANESCO hakikisheni mnafanya marekebisho kwenye transfoma zote nchini hatuwezi kuona transfoma ya milioni 20 linaharibika kwa ajili ya kifaa cha shilingi 500,000,”amesema Judith.

Ameongeza kuwa kitendo cha kukosekana vifaa vya ulinzi kwenye mifumo ya transfoma kunasababisha uharibufu na usumbufu kwa wananchi.

“Kwa sababu tunapitia changamoto ya upungufu wa umeme basi mnataka kupitia humo kuleta sababu kumbe changamoto nyingine mnazijua ni kitendo cha kuwajibika,” amesema.

Ameongeza kuwa nyakati zimebadilika hivyo wanapaswa kujitathimini na kufanyakazi kwa weledi ili kuwapunguzia lawama mafundi na mameneja wa wilaya na mikoa.

Aidha amekitaka kitengo cha manunuzi kupitia upya sheria na mikataba kwa wakandarasi wanaowapa tenda ya vifaa ikiwezekana kuwapa miezi sita baada ya miaka miwili ili wakionyesha ucheleweshaji wa kuleta vifaa ninkuachana nao na kutafuta wengine.

Naye Mkurugenzi wa TANESCO Kanda ya Mashariki, Mhandisi Keneth Boimanda amesema maelekezo yaliyotolewa watayafanyia kazi kwa haraka.

“Maelekezo tumeyapokea tutakaa wote mainjinia na mafundi kuhakikisha tunatekeleza maagizo haya ya kuzifanyia marekebisho transfoma zote zenye hatari ya kuharibika”amesema Mhandisi Boimanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amesema TANESCO wanapaswa kuwajibika na si kutupiana mpira hivyo kama wilaya watasimamia ili kuona utekelezaji wa maboresho kwenye transfoma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles