23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

TANESCO wameshindwa kuzalisha umeme – Muhongo

muhongo_clipNA FLORENCE SANAWA, MTWARA

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limeshindwa kuzalisha umeme na kusababisha Kiwanda cha Saruji cha Dangote kukodi genereta 75 kutoka nchini China kwa ajili ya kuzalisha umeme wa megawati 42.

Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku moja mkoani hapa, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema shirika hilo limeshindwa na halina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 45 zinazohitajika kwa uzalishaji kiwandani hapo.

“TANESCO wamekuwa wakizalisha umeme wa megawati 18 ambazo hazikidhi mahitaji ya uwekezaji.

“Lakini, kama Watanzania wanataka kufaidika na uwekezaji ni lazima Serikali iongeze uzalishaji wa umeme.

“Ukosefu wa umeme umewakera Watanzania na kwa kulitambua hilo, tumefuta likizo zote za wafanyakazi ili tufanye kazi na kusimamia ipasavyo uzalishaji wa umeme,” alisema Profesa Muhongo.

“Hata ukiangalia wawekezaji wetu ni aibu mtu anataka umeme anakosa anataka makaa ya mawe anakosa wakati hivi vitu vipo hakikisheni mnakaa na mwekezaji huyu mnazungumza ili kupata mwafaka nae” alisema Prof. Muhongo.

Naye Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Ufuaji Umeme wa TANESCO, John Mageni, alisema shirika hilo liko katika
mchakato wa kuongeza uzalishaji wa umeme ifikapo Machi mwakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles